Zuchu ametajwa kati ya wasanii 10 wanaopigiwa upato kushamiri mwaka huu mpya wa 2021.

Mwanamuziki anayechipuka, kutoka Tanzania Zuchu ametajwa kati ya wasanii 10 wanaopigiwa upato kushamiri mwaka huu mpya wa 2021.


Zuchu @officialzuchu alitambulishwa kwetu na nyota wa bongo fleva Diamond Platinumz @diamondplatnumz, na Wasafi amekonga nyoyo za kizazi kipya cha mashabiki wa Afro Beats kutokea Tanzania hadi Afrika kwa jumla.

Mwanamuziki huyu huimba kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza na ana sifa za muziki wa Tanzania aina ya Bongo Fleva.


Alitangaza kuwasili kwenye jukwaa la muziki kwa albamu yake ya I AM Zuchu chini ya Lebo ya kurekodi muziki ya WCB Wasafi @wcb_wasafi

Kwa mujibu wa programu ya kupakua muziki ya Boomplay, albamu yake ndio iliochezwa sana nchini Tanzania mwaka 2020.


Aidha video za muziki wake zimefanikiwa kuvutia mamilioni ya mashabiki katika mtandao wa YouTube.

Watumbuizaji wengine ni Elaine, Fik Fameica kutoka Uganda,Kabza De Small (Africa Kusini) Kidi kutoka Ghana, Omah Lay kutoka Nigeria.

Sha Sha (Zimbabwe),Soraia Ramos (Cape Verde),Tems (Nigeria),Elaine ( Afrika Kusini) wanakamilisha orodha hiyo ya wanamuziki 10.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*